August 2, 2017 millardayo.com imekukusanyia uchambuzi wa Magazeti kutoka kwenye twitter @millardayo ikiwa ni uchambuzi wa Habari zote kubwa kupitia Magazeti yaliyoandikwa leo Tanzania ambapo hizi ni baadhi ya Habari kubwa zilizoandikwa leo.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA kimeanzisha mpango maalumu wenye lengo la kutoa mafunzo yanayolenga kuwainua wanawake kiuchumi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na Asasi ya kiraia ya United Against Crime imezindua Namba mpya 114 kupiga wakati wa majanga.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA kimeanzisha mpango maalumu kutoa mafunzo yanayolenga kuwainua wanawake kiuchumi. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
41% ya watoto chini ya miezi 6 wapo hatarini kupata utapiamlo na magonjwa yatokanayo na taratibu zisizofaa kulisha watoto. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likishirikiana na Asasi ya United Against Crime imezindua No mpya 114 kupiga wakati wa majanga. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Kampuni za kuuza, kusambaza gesi ya kupikia zimetakiwa kufunga mitambo ktk Taasisi za Serikali kupunguza ukataji wa miti. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Wabunge 8 wa Viti Maalum wa CUF leo wanaanza kupigania nafasi zao Makahamani ikiwa ni wiki moja tangu kuvuliwa uanachama. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), umeomba kuongeza nauli ya vivuko vya Magogoni-Kigamboni kwa abiria, pikipiki na Bajaj. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Watu 1,236 mkoani Kilimanjaro wamegundulika kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) katika kipindi cha kuanzia Jan hadi Jun, 2017. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Imeelezwa kuwa licha ya zaidi ya 97% ya wanawake nchini kunyonyesha watoto lakini wengi hawanyonyeshi kwa utaratibu ulioshauriwa. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
"Ni jambo lisilopendeza kuchukua fedha za maendeleo kwa ajili ya kuhudumia wafungwa." – Waziri Mwigulu Nchemba. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Baada ya kuona sehemu kubwa ya kuzikia imejaa Halmashauri ya Jiji la D'Salaam imetenga Tsh. Mil 500 kununua maeneo ya kuzikia. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Mbunge wa Hanan'g Dr Mary Nagu (CCM), amesema hajawahi kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa Polisi kwa agizo la DC wa Hanan'g. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini mkataba wa makubaliano ya awali kupeleka umeme vijiji vya mpakani mwa nchi hizo. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imewahukumu watu wawili kifungo cha miaka miwili jela kwa kukutwa na sare za Jeshi la Polisi bila kibali. #UHURU
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Hospitali za mikoa zimeagizwa kujenga vituo vya kutolea huduma ya Methadone kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa dawa za kulevya. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Idara ya Uhamiaji Tanzania imefanya msako katika viwanda na maeneo mbalimbali nchini na kufanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 5,700 #UHURU.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Serikali imewataka wananchi kuachana na maneno ya wanasiasa badala yake wafanye kazi kwa kuwa Taifa linajengwa na wao wenyewe. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Raia 2 wa DRC wanashikiliwa na Polisi Rukwa kwa kukutwa na masanduku ya vipande 15 vya mawe na mchanga unaosadikiwa kuwa madini. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Jeshi la Polisi Z'bar linawashikilia watu 44 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kumshambulia kondakta wa daladala na kupata ulemavu. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Watumishi wa Umma waliodanganya wamefika Form 4 na wasioviwasilisha kwa waajiri wao wakiwemo wa Darasa la 7 wameanza kuondolewa. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Serikali imesema uchumi wa Tanzania uko imara na umekuwa ukiongoza kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (AEC). #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Jeshi la Magereza limetakiwa kuwatumia wafungwa ktk shughuli za kilimo na ufugaji ili kukidhi mahitaji yao ikiwemo chakula. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Imeelezwa kuwa jumla ya Shule 402 katika Mkoa wa Dar es Salaam hazina ofisi za Walimu jambo linaloathiri utoaji wa elimu bora. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
TAKUKURU Mkoa wa Mara imemfikisha Mahakamani Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyambitilwa kwa kudai na kupokea rushwa Tsh. 30,000. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Taasisi za Serikali zimeagizwa kuacha matumizi ya mkaa na kuni ili kupunguza ukataji miti badala yake zitumie nishati mbadala. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa moyo waliokuwa wanasafirishwa kwenda kutibiwa nje ya imepungua kwa 80%#HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
ULIPITWA? CHADEMA kuhusu hali ya Uchumi wa nchi, imetaja vigezo vitano…tazama kwenye video hii!!!
ULIPITWA? Serikali imewajibu wanaosema uchumi wa Nchi umeporomoka…play kwenye video hii!!