Baada ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa shirikisho la soka Tanzania TFF Revocatus Kuuli kutangaza matokeo na wengi kusikika wakipongeza kutokana na kuamini mchakato huo uliendeshwa kwa uhuru na haki.
Ayo TV imefanikiwa kumpata mchezaji wa zamani na mchambuzi wa masuala ya soka Ally Mayay Tembele ambaye alikuwa ni miongoni mwa wagombea sita wa nafasi za Urais, vipi kwa upande wake ameridhishwa na matokeo.
“Uchaguzi nimeridhishwa na matokeo kwa sababu katika demokrasia ni kitu ambacho kinatokea hamuwezi kufanana mitazamo, wewe unaweza ukaona hivi mwingine akaona vile sasa unapokuja kugombea ni lazima uwe umejiandaa kupokea chochote” >>> Ally Mayay
Alichokiagiza waziri Mwakyembe baada ya kutangazwa matokeo ya Urais na makamu TFF