Winga mshambuliaji wa zamani wa club ya Azam FC ambaye kwa sasa anaichezea club ya Tenerife ya Hispania Farid Musa, amewasili Tanzania August 30 na leo alifanya mazoezi na wenzake wa Taifa Stars kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Botswana September 2.
Farid Musa baada ya mazoezi tumempata katika interview na kumuuliza kuhusu maendeleo yake Hispania, awali alikuwa anacheza team B vipi amepandhishwa? kuhusu kucheza LaLiga na timu yake ya Tenerife je?
“Hispania nimejifunza kitu kimoja uvumilivu mara ya kwanza nilivyoenda kule uvumilivu maana nilikuwa mnyonge ukizingatia wenzetu wanaongea lugha tofauti iliniwa vigumu sana kujifunza lugha yao na jinsi wanavyoishi”>>> Farid Musa
“Mwalimu aliyenichukua Tenerife B alinifundisha mengi na yeye ndio alichangia mimi hadi sasa hivi nimepandishwa timu ya wakubwa, japo haikuwa nzuri kwangu mechi ya kwanza ya Real Zaragoza nilitakiwa nianze ila vibali kutoka chama cha mpira cha Hispania havikuwa vimetoka” >>> Farid Musa
“Nashukuru wameliona hilo na mchango wangi karibuni tu watanzania wataniona nacheza Ligi kubwa ya Hispania kama sasa hivi timu yetu imefanya vizuri tumecheza mechi mbili tumeshinda zote tuna point sita na mwalimu ameahidi atapandisha timu”>>> Farid Musa
Kama utakuwa unakumbuka vizuri club ya Tenerife ya Hispania anayoichezea Farid Musa ilikuwa ipande kucheza Ligi Kuu Hispania msimu wa 2017/2018 endapo ingeshinda game yake ya pili ya marudiano, hivyo wanapamba msimu huu katika Segunda kupanda msimu ujao.
Samatta kaipata ofa ya kumrithi Van Persie? ukimuuliza atakujibu hivi