Jumamosi ya August 26 2017 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam wekundu wa Msimbazi Simba walicheza game yao ya kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 dhidi ya Ruvu Shooting na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 7-0.
Ushindi wa Simba ulipatikana kuanzia dakika ya 18 baada ya Emanuel Okwi kufunga goli la kwanza dakika 18 na baadae dakika ya 22, 35, 52 akafunga goli lake la nne katika ushindi huo wa 7-0.
Baada ya kufunga hat-trick dakika ya 35 Okwi alishangilia kwa kuweka mpira tumboni, ishara ambayo wachezaji wengi ushangilia kama ishara ya mpenzi wake kuwa mjamzito, vipi kwa Okwi amemaanisha nini?
“Nashukuru wachezaji wenzangu wamenisaidia kufunga magoli manne tunachoangalia mchezo unaofuata, leo kweli ningependa kuwapongeza wachezaji wenzangu ambao tumetumia nafasi ambazo tumetengeneza, nimeweka mpira tumboni kwa sababu mke wangu mjamzito hivyo ni zawadi ya mtoto wetu anatakayezaliwa” >>> Okwi
VIDEO: Hat-Trick ya Okwi iliyookoa Tsh milioni 5 za Haji Manara