November 5 2017 Ligi Kuu England iliendelea kwa michezo kadhaa kuchezwa ikiwemo big match za Chelsea dhidi ya Man United iliyomalizika kwa Chelsea kupata ushindi wa goli 1-0, goli likifungwa na Alvaro Morata dakika ya 55 kwa kichwa.
Big Match nyingine ilichezwa katika uwanja wa Etihad kati ya wenyeji Man City wakicheza dhidi ya Arsenal, game ambayo ilimalizika kwa Man City kupata ushindi wa magoli 3-1, magoli ya Man City yakifungwa na Kelvin De Bruyne dakika ya 19, Sergio Aguero kwa penati dakika ya 50 na Gabriel Jusus dakika ya 75.
Arsenal wakipata la kufutia machozi kutoka kwa Alexandre Lacazette dakika ya 65, ushindi huo sasa umeifanya Man City kuenelea kuwa kileleni mwa msimamo wa EPL kwa kuwa na point 31 wakati Chelsea wakiwa nafasi ya nne kwa kuwa na point 22.
Manara kabeba TV na kuja nayo kwa Waandishi leo kuonyesha Simba inavyoonewa (+video)