Staa wa soka wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo usiku wa December 7 2017 amefanikiwa kutangazwa mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or na kuwashinda Lionel Messi wa FC Barcelona na Neymar wa Paris Saint ya Germain ya Ufaransa.
Tuzo hiyo imezidi kudhihirisha kuwa Ronaldo ni moja kati ya wachezaji bora wa muda wote katika soka, hiyo inatokana na kujizolea tuzo kubwa ikiwemo ile ya mchezaji bora wa FIFA aliyoshinda mwezi October mwaka huu 2017.
Ronaldo ameshinda tuzo ya tano ya Ballon d’Or akiwa na Real Madrid lakini tuzo yake ya kwanza ya Ballon d’Or inayoandaliwa na France Football Magazine alishinda mwaka 2008 akiwa amefunga jumla ya magoli 42, akitwaa Champions League na taji la Ligi Kuu England EPL.
Hata hivyo Ronaldo ameeleza nia yake ya kutaka kushinda Ballon d’Or mara saba na kupata watoto saba ndio malengo yake kama ambavyo anatumia namba saba uwanjani lakini pia ni nembo yake ya biashara.
VIDEO: Atayofanya Mo Dewji kwa Simba ndani ya mwaka mmoja