Baada ya kufanyika kwa mafanikio makubwa michuano ya soka la mchangani maarufu kama Ndondo Cup kwa mikoa ya Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam, waandaaji wa michuano hiyo wakiwa jijini Mbeya wametangaza kuandaa Ndondo Super Cup.
Kamati ya mashindano ikiwa jijini Mbeya imetangaza rasmi uwepo wa mashindano ya Ndondo Super Cup ambayo itafanyika jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha Mabingwa wa mikoa ilipofanyika michuano ya Sports Extra Ndondo Cup, akizungumza na vyombo vya habari mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Shaffih Dauda ametangaza kuwa hicho ni kilele cha Ndondo Cup 2017 kabla ya kuanza Ndondo Cup 2018.
“Mashindano hayo yatashirikisha timu nne na kutakuwa na michezo minne itakayofanyika tarehe 17, 18, 20, 21 mwezi February 2018 jijini Dar es Salaam”>>> Shaffih Dauda
Kwa upande wa mwenyekiti wa Ndondo Super Cup Gipson George amesifia hatua hiyo iliyofanywa na Clouds Media ukizingatia ujio wa Rais wa FIFA nchini Tanzania Infantino
“Hakuna asiyejua Rais wa FIFA atakuwepo hapa, hii ni heshima kubwa tuliyopewa duniani lazima na sisi tuwaoneshe na kuthamini ujio wao, Shaffih Dauda amewasiliana na viongozi wa TFF ili kuona namna ya fainali ya Ndondo Super Cup ikaja kutembelewa na Rais wa FIFA ndio maana tumeiweka February 21”>>>> Gipson George
Michuano ya Ndondo Super Cup yatashirikisha jumla ya timu nne ambazo ni Bingwa wa Mwanza Mnadani FC, Bingwa wa Mbeya Itezi United, Bingwa wa Dar es Salaam Misosi FC na Goms United akiingia kwa heshima ya mkoa wa Dar es salaaam kuwa ndio waasisi wa Ndondo Cup.
Alichokiandika Jerson Tegete baada ya Nyosso kumpiga shabiki