Kwenye semina ya fursa mwishoni mwa 2013 Dar es salaam ambayo mgeni rasmi alikua Rais Kikwete, Managing Director wa Clouds Media group Joseph Kusaga alitangaza kuhusu Clouds media group kupata kibali na kuwa kituo cha kwanza kwa kiafrika kupata kibali cha kurushia matangazo yake kutoka Abu Dhabi.
Pichaz mbalimbali unazoziona hapa ni za ofisi za Clouds TV International Abu Dhabi na haya mambo saba hapa chini ameyasema Mr. Kusaga kuhusu hii Clouds TV International.
1. Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyenzi Mungu kutuwezesha kufika hapa, hakuna Mungu kama yeye.
2. Naishukuru timu yangu nzima ya Clouds kwa ubunifu wa ajabu walionao.
3. Ulimwengu wa sasa hivi ni ulimwengu wa teknolojia… sisi kama Clouds tumesogea mbele na sasa tumebarikiwa kwa sababu ya jitihada, tunakua Television ya kwanza ya Kiafrika kurusha matangazo yake kutokea nchi za kiarabu na tutapiga katika boxes milioni 320, kitu ambacho sio cha kawaida.
4. Kwenye nchi za Kiarabu hakuna Television yoyote ya Kiafrika, kuna za Kihindi, Kifilipino, Kirusi na wengine lakini sisi tuliona nafasi hii, kwa nini tusiitumie? manake Waafrika wanazidi kuongezeka kufanya kazi na kuishi kwenye nchi za kiarabu lakini hawana kitu cha kuwawezesha kuona habari zao za nyumbani, burudani na mengine kutoka nyumbani.
5. Sio Watanzania tu, Waafrika wote wanaweza kuweka vipindi vyao… ukiwa wewe ni mbunifu unaweza kuweka content yako kwa bure au ikalipiwa kwenye kinga’muzi hiki, ikilipiwa unaweza kupata pesa yako kwa uwazi kabisa.
6. Mungu akipenda tumeamua kwamba mwezi wa nne 2014 tuwe tumekwenda hewani… lakini majaribio yameshaanza tayari.
Mr. Joseph Kusaga na Mtangazaji wa michezo Shaffih Dauda kwenye ofisi za Clouds TV International Abu Dhabi.
7. Wazo lililokuwepo toka mwanzoni ilikua ni Clouds TV International iwe media kubwa Afrika nzima kutokea Tanzania, ila kwa sisi Watanzania inakua ngumu ukifikiria kwamba unawezaje kutoka wewe Mtanzania kutoka nchi masikini alafu ukataka kwenda kumuuzia Mnigeria, kumuuzia Msouth Afrika na wengine… ilikua ngumu ndio maana tukaona tutokee Abu Dhabi.
8. Kwa heshima ambayo ipo kwa sasa, umoja wa falme za kiarabu (U.A.E) ndio imekua hub ya kila kitu, Abu Dhabi inaheshimika kifedha na kiustaarabu hivyo tuliingia makubaliano na serikali ya Abu Dhabi kupitia media zone yao iitwayo twofour54.
9. Unajua tena nchi za kiarabu zinavyopenda kusifika kwa kuwa wa kwanza kufanya jambo, mfano jengo kubwa kuliko yote duniani… hivyo serikali ya Abu Dhabi ikakubali kutubeba na kuwa kituo cha kwanza cha kiafrika katika nchi za kiarabu na kukubali kutusaidia kwa kila hali kiteknolojia.
10. Kuhusu ishu ya OTT (over the top) hii ni online zaidi, kwenye internet unafungua na unaangalia na tulichoweza kufanikiwa ni kuzishawishi nchi nyingi za Afrika kwamba kila nchi ya Kiafrika iwe ina nafasi ya kuwa na box lake, yani Kenya box, Congo Box, na sasa tayari Rwanda box imeshaanza kufanya kazi… kila nchi ya kiafrika itakua na box lake na sisi Waafrika wote tutajumuika wote kwenye box moja lililobeba yote hayo kwa hiyo kama Mkenya yuko Ukrain, Urusi au kwengine… akiingia kwenye internet tu anapata nafasi kuona box la nchi yake.
Shaffid Dauda na mkuu wa vipindi Clouds FM Sebastian Maganga wakipewa maelekezo ya jinsi kazi inavyofanyika.
Stuart Kambona kutoka Primetime Promotions na Shaffih Dauda kwenye moja ya studios.