Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 imeendelea leo kwa michezo miwili kuchezwa Azam FC wakiwa Songea kucheza dhidi ya Majimaji wakati Simba SC wakiwa uwanja wa Taifa DSM wakicheza dhidi ya Singida United.
Mchezo wa Simba dhidi ya Singida United ulikuwa unatajwa kuwa na ushindani zaidi kutokana na timu hizo zote kuwa zinawania nafasi za juu, Simba kuwepo nyumbani kumeisaidia kupata ushindi wa magoli 4-0, magoli ya Simba yakifungwa na Shiza Kichuya dakika ya 3, Asante Kwasi dakika ya 24 na Emmanuel Okwi aliyefunga magoli mawilu dakika ya 75 na 82.
Ushindi wa Simba sasa unaifanya Simba kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha jumla ya point 29 wakifuatiwa na Azam FC waliyopo nafasi ya pili kwa point 27 wakati Singida United wao watakuwa nafasi ya nne baada ya kupoteza mchezo wa leo wakibaki na point 23 zao.
Simba ilivyoiadhibu Singida United 4-0 leo, magoli yote yapo hapa