Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea tena leo kwa wekundu wa Msimbazi Simba kuwa wageni wa Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, Simba waliingia Kambarage kucheza mchezo wao wa 18 wa Ligi Kuu.
Simba imekuwa ikipata tabu kupata matokeo ya ushindi kwa baadhi ya game katika uwanja wa CCM Kambarage dhidi ya Mwadui FC na wamejikuta wakiambulia sare mara kadhaa, mchezo wa leo licha ya Simba kufanikiwa kupata ushindi mfululizo ila leo wamepunguzwa kasi kwa kulazimishwa sare ya 2-2.
Game ilianza kwa dakika ya 9 Simba kupata goli la uongozi lililofungwa na nahodha wao John Bocco ambaye pia alishindwa kumaliza game kwa kuumia enka, David Luhende akaisawazishia Mwadui dakika ya 60 lakini Simba wakapata penati iliyofungwa dakika ya 74 na Emmanuel Okwi ambapo hilo ndio goli lake la kwanza Ligi Kuu msimu huu kufunga nje ya Dar es Salaam.
Wengi wakiwa wameamini kuwa Simba ataondoka na point tatu, mshambuliaji wa Mwadui FC Paul Nonga dakika 1 kabla ya game kumalizika akaisawazishia goli Mwadui FC na kuufanya mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2, sare hiyo sasa inafufua matumaini kwa timu za Yanga, Azam FC na Singida kuendelea kupambania Ubingwa, hii ni sare ya sita ya Simba leo.
VideoMAGOLI: Yanga vs Majimaji FC Feb 14 2018, Full Time 4-1