Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 iliendelea tena leo Septemba 11 2016 kwa wekundu wa Msimbamzi Simba kuwakaribisha wakatamiwa wa Manungu Turiani klabu ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kucheza mchezo wa nne wa Ligi Kuu Tanzania bara.
Simba imeshuka dimbani kucheza Mtibwa Sugar ikiwa na kumbukumbu ya kuifunga goli 1-0 msimu uliopita nyumbani na ugenini, kabla ya leo Septemba 11 2016 kuibuka na ushindi wa tatu wa goli 2-0 na kufanya hicho kuwa kipigo cha tatu mfululizo kwa Mtibwa Sugar kufungwa na Simba katika VPL.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa timu zote mbili kabla ya kipindi cha pili Simba kuja na mbinu mbadala iliyoifanya Mtibwa kufungwa goli la kwanza dakika ya 52 kupitia kwa Ibrahim Ajib na baadae Laudit Mavugo akafunga goli la pili dakika ya 66.
Matokeo ya mechi nyingine ya VPL iliyochezwa leo Septemba 11 2016
- Tanzania Prisons 1-0 Toto Africans
Msimamo wa VPL baada ya mechi za Septemba 11 2016. pic.twitter.com/8uJlKzeYwG
— millard ayo (@millardayo) September 11, 2016
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0