Shirikisho la soka barani Africa CAF leo Jumatano ya November 1 2017 limetaja majina ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa mwaka 2017.
Katika list ya majina 30 yaliotangazwa leo na shirikisho la soka Afrika nahodha wa taifa stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ametajwa katika list kwa mara nyingine tena.
Mbwana Samatta ametajwa katika list hiyo na ya wachezaji wengine wakubwa Afrika kama Eric Bailly wa Manchester United, Mohamed Salah wa Liverpool, Pierre-Emerick Aubameyang wa Borussia Dortmund, Sadio Mane wa Liverpool, Victor Moses wa Chelsea.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri hii ni mara ya pili kwa Samatta kutajwa katika list hiyo lakini amewahi kushinda tuzo tuzo ya mchezaji bora Afrika mwaka 2015 kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika akiwa na TP Mazembe.
Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2017 sherehe zake zitafanyika Alhamisi ya January 4 2017 nchini Ghana katika jiji la Accra, kama hufahamu mchezaji bora wa Afrika mshindi anapatika kwa kupigiwa kura na makocha wa timu za taifa, wakurugenzi wa ufundi wa mashirikisho ya soka Afrika ambayo ni mwanachama wa CAF.
Manara kabeba TV na kuja nayo kwa Waandishi leo kuonyesha Simba inavyoonewa (+video)