Leo August 2, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania imeanza kusikiliza kesi ya Wabunge 8 wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi CUF waliovuliwa Uanachama na Prof. Lipumba hivyo kupoteza sifa ya kuwa Wabunge.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo, maombi yanayosikilizwa ni zuio la Utekelezaji wa mchakato wa kuwaapisha Wabunge Wateule wa CUF pamoja na kuzuia utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza Kuu la CUF.
Kesi iliyofunguliwa na Wabunge 8 wa Viti Maalumu kupinga kuvuliwa uanachama na CUF imeanza kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania. pic.twitter.com/3AGGBKaWOe
— millardayo (@millardayo) August 2, 2017
ULIPITWA? Prof. Lipumba baada ya Spika kuridhia Wabunge 8 kuvuliwa uanachama CUF…bonyeza PLAY kutazama kwenye VIDEO hii!!!