Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo Jumamosi ya September 2 2017 imecheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliyopo katika kalenda ya FIFA dhidi ya timu ya Botswana uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Tanzania leo imefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Botswana, magoli ambayo yamefungwa na Simon Msuva dakika ya 5 baada ya kutumia assist safi ya Mzamiru Yassin lakini Msuva akafunga tena dakika ya 61 kwa assist safi ya Shiza Kichuya.
Taifa Stars leo imecheza na Botswana ambao wapo nafasi ya 140 katika viwango vya FIFA Tanzania ikiwazidi kwa nafasi 20, kwani Tanzania wao wapo nafasi ya 120, hivyo Botswana ambao wanafungwa kwa mara ya pili na Taifa Stars kwa mwaka 2017 walitaka kulipa kisasi.
Ushindi huo utaiwezesha Tanzania ambayo ipo nafasi ya 120 katika viwango vya FIFA izidi kupanda lakini kama utakuwa unakumbuka vizuri Taifa Stars mara ya mwisho ilicheza na Botswana Uwanja wa Taifa March 25 2017 na kufungwa magoli 2-0, magoli yote yalifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 2 na 87.
Samatta kaipata ofa ya kumrithi Van Persie? ukimuuliza atakujibu hivi