AyoTV imefanikiwa kumpata staa wa Bundesliga katika Exclusive Interview anaitwa Yussuf Yurary Poulsen anayecheza Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga) ambaye ana asili ya Tanzania, kama humfahamu vizuri Yussuf Yurary Poulsen anacheza Ligi Kuu Ujerumani katika club ya RB Lipzig.
Timu ya RB Lipzig ambayo anacheza Yussuf imemaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Ujerumani msimu wa 2016/2017 Bingwa akiwa Bayern Munich halafu Borussia Dortmund ikishika nafasi ya tatu, Yussuf Poulsen alikuwa Tanzania jijini Tanga kwa bibi yake mzaa baba.
Baba yake mzazi Yussuf mzee Yurary alifariki kwa kansa wakati Yussuf akiwa na umri wa miaka 6, mama yake ni raia wa Denmark, Yussuf Poulsen wengi tumemfahamu hivi karibuni baada ya mafanikio yake Bundesliga lakini ana asili ya Tanzania, AyoTV imemnasa kwenye exclusive interview.
Vipi ni mara yake ya kwanza kuja Tanzania? kwa nini ameamua kucheza timu ya taifa ya Denmark upande wa mama yake na sio Tanzania licha ya kuwa alikuwa na nafasi pia ya kuchagua kucheza Tanzania sehemu ambayo ni nyumbani kwa baba yake mzazi?
“Hapana hii sio mara ya kwanza kuja Tanzania baba yangu ni mtu mwenye asili ya hapa nilikuja nikiwa mdogo mwaka 1996, 2002 lakini pia nilikuja tena 2008 na 2011, historia yangu nimezaliwa kwa baba mtanzania na mama mdenmark na nimekuwa nikipenda kucheza mpira katika maisha yangu yote”
“Kwanza ilikuwa faraja kwangu kucheza timu iliyokuwa daraja la kwanza Denmark mwanzoni na kucheza kwa msimu mzima, kuhusu kwani nini sikucheza timu ya taifa ya Tanzania? ni swali zuri lakini kiukweli sikupokea ofa kutoka Tanzania ya kucheza timu ya taifa lakini pia sijui ingekuwaje kama ofa ingekuja”
“Nimecheza timu zote za vijana za taifa za Denmark na sasa timu ya wakubwa lakini sikuwahi kufikiria kama ningepata nafasi ya kucheza timu ya taifa ya wakubwa ya Denmark hadi nilivyoitwa lakini nimezaliwa na kukulia Denmark kama nilivyosema awala kama ofa ya Tanzania ingekuja sijui ningechagua kucheza timu gani”
Yussuf Poulsen anacheza timu ya taifa ya Denmark lakini ana asili ya Tanzania, kwa upande wa baba yake alikuwa akifanya kazi katika meli ya makontena iliyokuwa inatoka nchi za Afrika kwenda Denmark, Poulsen alizaliwa mwaka 1994 Copenhagen Denmark na msimu ujao 2017/2018 tutamuona kwa mara ya kwanza akicheza Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA Champions League.
VIDEO: Taifa Stars ilivyopokelewa, Kocha Mayanga kathibitisha wamemuacha mchezaji South