Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 imeendelea leo Jumapili ya January 14 2018 kwa game mbili kuchezwa, AFC Bournemouth walikuwa ni wenyeji wa Arsenal wakati game yenye mvuto zaidi EPL kwa leo ilikuwa ni game ya Man City dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Liverpool walikuwa wenyeji katika uwanja wao wa Anfield dhidi ya Man City ambayo kabla ya game ya leo Man City ilikuwa haijapoteza mchezo hata mmoja, hatimae Liverpool imevunja mwiko huo na kuwa timu ya kwanza kuifunga Man City katika EPL msimu huu.
Man City baada ya kucheza michezo 22, walikuwa wametoka sare mchezo mmoja na kushinda michezo yote lakini leo kipigo cha goli 4-3 kutoka kwa Liverpool kinavunja rekodi yao, magoli ya Liverpool yamefungwa na Chamberlaine dakika ya 9, Firmino dakika ya 60, Mane 62 na Mohamed Salah dakika ya 68.
Baada ya kuwanyuma Man City walirudi mchezo na kufanikiwa kufunga magoli kupitia kwa Sane dakika ya 41, Bernardo Silva dakika ya 84, Ilkay Gundogan dakika ya 92, licha ya Man City kubadili mchezo na kufanikiwa kumiliki mpira kwa asilimia 65 kwa 35 lakini hawakuweza kusawazisha.
Rekodi aliyoiweka Guardiola baada ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwezi