Azam FC Jumamosi ya January 27 2018 walikuwa wenyeji wa Yanga kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu uliyochezwa uwanja wa Chamazi, huo ulikuwa ni mchezo wa kukamilisha round ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania bara kwa Yanga na Azam FC.
Siku chache kabla ya mchezo kuchezwa Azam FC walilalamika kuhusu refa aliyewachezesha Israel Nkongo kutokuwa na imani nae, hivyo baada ya game kumalizika kwa Azam FC kupoteza kwa magoli 2-1, huku mchezaji wa Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kuoneshwa kadi nyekundu.
Nahodha wao Himid Mao aliongea na Azam TV na kuulizwa kuhusu game hiyo na kiwango cha muamuzi kwa upande wake amekionaje
“Sisi kufungwa nafikiri ni uzembe tu baada ya kupata goli tukaridhika nakujiona kama tushamaliza game na tukacheza mpira sana katika eneo letu na wenzetu ndio wakatumia hayo makosa na wakatuadhibu”>>> Himid Mao
“Ndio kabla ya mchezo tulikuwa hatukubaliani na muamuzi lakini hata katika game hii nilimfuata kama nahodha baada ya sisi kufanya faulo tatu za kwanza”>>>Himid Mao
“Haiwezekani faulo tatu una toa kadi tatu za njano bila kutoa onyo hakuna mpira wa hivyo duniani lakindi ndio mpira hatuwezi kumlaumu muamuzi lakini alichokifanya leo sio kitendo kizuri kabisa”>>>Himid Mao
Michuano ya Cricket Tanzania inaanza kesho January 28 2018
Alichokiandika Jerson Tegete baada ya Nyosso kumpiga shabiki