Baad ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya Yanga kutopata ushindi kwa michezo miwili mfululizo ya Ligi Kuu, January 21 2018 walirudi tena uwanjani kucheza mchezo wao wa 14 wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting.
Mchezo wa leo uliochezwa Taifa Yanga ndio alikuwa ugenini lakini licha ya kuwa Yanga walikuwa na mtaji mkubwa wa mashabiki hawakufanikiwa kupata ushindi wa magoli mengi na kuishia kupata ushindi wa goli 1-0 ambalo lilileta utata nani kafunga ni Buswita wa Yanga au Ruvu wamejifunga.
Ushindi wa leo wa Yanga wa goli 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting unakuwa ni ushindi wa 6 kati ya game zao saba walizokutana hivi karibuni, Yanga wakifunga goli la 17, katika mechi saba hizo Ruvu amewahi kutoka sare mara moja na kufunga goli moja.
VIDEO: Simba ilivyoiadhibu Singida United 4-0 leo, magoli yote yapo hapa