Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein ameweka wazi msimamo wake baada ya shauku ya wengi kutaka kusikia kutoka kwake ni nini msimamo wake baada ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kujadili muda wa uongozi.
Awali iliripotiwa kuwa Baraza la Mapinduzi Zanzibar lilijadili kuhusiana na kuongeza muda wa utawala wa Rais, jambo ambalo wengi walitaka kufahamu kwa Rais wa Zanzibar Ali Shein analichukuliaje, Shein akiongea na Azam TV amefunguka na kueleza kuhusiana na hilo.
“Muda wangu ukiisha nitaondoka haraka sana hakuna atakayenilazimisha mimi nibaki sheria mimi naijua na katiba naijua, hilo walizungumza wawakilishi barazani wana haki ya kuzungumza kwa mujibu wa sheria zao na taratibu zao na haki yao kuzungumza”>>>Shein
“Mimi nimesikia mmoja akiwa anazungumza kuwa anauzoefu kuna nchi nyingi duniani kuwa wana muda wa miaka saba ya utawala wengine miaka mitano akasema kwa nini na sisi tusifanye saba?”>>>Shein
“Haikusudiwi kwamba mimi nisitoke ndio iwe saba labda baadae lakini sidhani kama hilo lipo mimi sijalisema na sitalisema hata siku moja, siku yangu ikifika nitamwambia mama Shein twenzetu”>>>Shein
“Macho yako ni balaah, shingo yako sijawahi kuona”