Club ya Dar es Salaam Young Africans leo Jumamosi ya February 10 2018 ilicheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya mtoano wa michuano ya club Bingwa Afrika dhidi ya club ya St Louis ya Ushelisheli.
Yanga wakiwa uwanja wa Taifa dhidi ya wageni wao St Louis walifanikiwa kupata ushindi mdogo wa goli 1-0 tofauti na matarajio ya wengi, Yanga licha ya kupata mkwaju wa penati dakika za mapema kipindi cha kwanza, Obrey Chirwa aliipiga nje na kuufanya mchezo kuzidi kuwa mgumu kutoka na St Louis kucheza kwa kujihami zaidi.
Baada ya mambo kuwa magumu kocha George Lwandamina wa Yanga alifanya mabadiliko dakika ya 66 kipindi cha pili kwa kuwatoa Ibrahim Ajibu na Emmanuel Martin na kuwaingiza Juma Mahadhi na Geofrey Mwashiuya mabadiliko ambayo yalizaa matunda dakika ya 67 ikiwa ni mpira wa pili Juma Mahadhi anagusa na kuifungia Yanga goli la ushindi.
Kwa upande wa Chirwa aliyekosa penati katika mchezo wa leo anaweka rekodi mbaya baada ya leo kukosa penati yake ya tatu kati ya tano alizopiga katika kipindi cha miezi miwili, Chirwa alikosa penati vs URA Mapinduzi Cup, akakosa dhidi ya Ihefu FC na akashinda moja, akafunga dhidi ya Njombe Mji na leo dhidi ya St Louis, kwa matokeo hayo Yanga watahitaji ushindi au sare ya aina yoyote katika mchezo wa marudiano ili wasonge mbele.
VIDEO: Simba imetangaza kumpeleka Haruna Niyonzima India