Jumamosi ya July 8 2017 kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka Tanzania TFF baada ya kuvunjwa na kuundwa tena ilikaa kikao chake cha kwanza na kufanya usaili wa wagombea wa nafasi mbalimbali watakaogombea katika uchaguzi mkuu wa TFF utakaofanyika August 12 Dodoma.
Baada ya kufanywa usaili wagombea kadhaa walikatwaa akiwemo Rais wa sasa wa TFF Jamal Malinzi kwa kushindwa kuwepo katika usaili lakini pia alikatwa mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji kanda ya Dar es Salaam kocha wa zamani wa Simba na Mwadui FC Jamhuri Kiwelu Julio kwa madai ya kushindwa kuthibitisha kuwa na cheti cha kidato cha nne.
AyoTV imempata katika exclusive interview Julio ni kweli hana cheti cha kidato cha nne? “Baada ya kuulizwa swali kuhusu cheti changu nikawaambia kuwa kimepotea lakini niligombea makamu wa Rais wa Simba na walienda kuthibitisha NECTA kuwa nimemaliza kidato cha nne sasa sioni sababu ya kuenguliwa hapo kisa cheti” >>>Julio
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1