Baada ya siku tatu kupita toka Mahakama ya juu nchini Kenya itangaze kufuta matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Kenya uliyofanyika August 8 2017 na Rais Uhuru Kenyata kufanikiwa kuibuka mshindi mbele ya Raila Odinga, leo tume ya uchaguzi Kenya IEBC imetangaza tarehe ya uchaguzi mpya wa marudiano.
Kwa mujibu wa katiba ya Kenya matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Kenya baada ya kutangazwa kufutwa na Mahakama ya juu, sheria au katiba ya Kenya inataka uchaguzi Mkuu kurudiwa ndani ya siku 60, hivyo leo tume ya uchaguzi Kenya IEBC imetangaza kuwa October 17 2017 ndio tarehe ya uchaguzi wa marudio.
Pamoja na kuwa wizara ya elimu Kenya kuomba muongozo wa tarehe hiyo kuingiliana na tarehe ya wanafunzi kufanya mitihani, tume imetangaza kuwa uchaguzi Mkuu hautaathiri ufanyaji wa mitihani wa wanafunzi.
ULIPITWA: CCM yaongelea maamuzi ya Mahakama Longido…tazama kwenye hii video!!