Ukuaji wa Sayansi na Teknolojia umepelekea mabadiliko katika sehemu nyingi ambapo kutokana na maendeleo Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA na Wizara ya Afya zimezindua Mkataba wa huduma kwa mteja toleo la tatu na namba ya msaada kwa mteja ikiwa ni moja ya njia ya kurahisisha mawasiliano baina yao na mteja zinapoiniwa bidhaa feki.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Hiiti Sillo amesema>>>”Kati ya 2012 hadi sasa kumekuwa na mabadiliko mengi yanayoathiri shughuli za udhibiti na vile vile wigo na aina ya huduma tunazozitoa kwa Wateja.
“Hii ni pamoja na kukua kwa biashara na bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA kutokana na mabadiliko na matumizi ya teknolojia mbalimbali, mabadiliko ya sera za kiuchumi, utandawazi, soko huria, sanjari na suala la milipuko ya magonjwa ambayo imepelekea bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA kuongezeka katika soko.” – Hiiti Sillo
TFDA yafafanuzi kuhusu Mchele wa Plastic unaodaiwa kusambaa Tanzania!!!