Taarifa zilizoenea mchana wa leo August 29 2017 katika soka ni kuhusiana na chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na kudai wapewe Tsh milioni 150.
AyoTV ilifanikiwa kufika eneo la tukio na kuongea na mmoja kati ya waliyokutana na tukio hilo ambaye ni katibu wa chama cha soka wilaya ya Ilala na katibu wa kamati ya mashindano ya DRFA mzee Daudi Kanuti na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Wakati leo naingia ofisini asubuhi nikakutana na jamaa akaniuliza wewe ndio Kanuti? nikaambiwa panda juu nikakuta wenzangu wamefungwa kamba nikaambiwa tulia, baadae wakatoka wakarudi na kamba wakanifunga kamba na wakanifungua pingu” >>>Kanuti
“Wakaniambia kaa chini halafu wakaniambia sikiliza sisi shida yetu pesa hapa kuna Tsh Milioni 150 tunaitaka hiyo pensa, nikawaambia hiyo pesa mimi napata wapi, wakanisachi wakachukua funguo na Tsh laki mbili halafu wakaanza kusachi ofisi na kuchukua Tsh 400,000”>>> Kanuti
Video ya dakika 2 ikionyesha Hat-Trick ya Okwi iliyookoa Milioni 5