Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa uamuzi wa kupokea ama kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji nyumbani kwa Wema Sepetu ifikapo October 4 2017.
Hatua hiyo inatokana na kuwasilishwa kwa pingamizi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kutoka kwa wakili wa utetezi , Peter Kibatala, kwamba kielelezo hicho kina mapungufu kisheria, hivyo kisipokelewe.
Katika hoja zake wakili wa serikali, Constantine Kakula amedai kuwa hati hiyo ipo sahihi, hivyo ipokelewe na Mahakama. Kutokana na maelezo hayo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi October 4, 2017 kwa ajili ya kutoa uamuzi.
Mbali ya Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas ambapo wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.
VIDEO: “Zitto utanifanya nini? naweza kukuzuia usiongee hadi mwisho wa Ubunge wako” – SPIKA