Club ya Ndanda FC ya Mtwara imekuwa club ya pili ya pili ya Tanzania kuanza kufanya utamaduni wa kuwa na siku maalum ya kutambulisha jezi, wachezaji na kufanya shughuli za kijamii kama ilivyokuwa kwa club ya Simba SC ambayo hufanya kitu kama hicho (Simba Day) kila mwaka August 8.
Ndanda FC ambao wametoka kupata udhamini mnono hivi karibuni utakaowawezesha kujiimarisha kiuchumi, watacheza mchezo wa kirafiki kesho uwanja wa Chamazi Dar es Salaam dhidi ya Ruvu Shooting ambapo hiyo itakuwa ni Ndanda Day kwa ajili ya mashabiki wa Dar es Salaam.
Uongozi wa club ya Ndanda FC wao wameamua kuwa na Ndanda Day mara mbili kwa mwaka, watakayokuwa wanaifanya Dar es Salaam na Mtwara ambapo ndio makao makuu na chimbuka la club yao, Ndanda Day kwa kesho itapambwa na TID, Amin, Juma Nature na Jay MO ambao ni wasanii wenye asili ya Mtwara.
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0