Baada ya weekend kuchezwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018, leo Jumanne ya January 30 2018 michezo ya Kombe la Azam Sports Federation iliendelea kama kawaida kwa michezo kadhaa ya round ya tatu kuchezwa katika viwanja mbalimbali.
Yanga walikuwa katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza dhidi ya wenyeji wao Ihefu FC, licha ya kuwa Ihefu FC inatokea daraja la kwanza lakini mchezo haukuwa rahisi kwa Yanga kupata ushindi na hatimae dakika 90 zilimalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1.
Ihefu FC ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la uongozi dakika ya 37 baada ya Andrew Vincent wa Yanga kujifunga lakini Yanga wakasawazisha dakika za nyongeza kwa mkwaju wa penati kupitia Obrey Chirwa, baada ya hapo mikwaju ya penati ikampa ushindi Yanga wa penati 4-3 na safari ya Ihefu FC ikaishia hapo.
VIDEO: Magoli ya John Bocco na Okwi yalivyoiua Majimaji FC leo