Ndio kwanza leo ni siku ya 15 toka tuuanze mwaka 2018 lakini kumaliza mwaka haimaanishi kuwa hatuwezi kuzungumzia ishu za mwaka 2017, katika pitapita zangu nimekutana na list ya wachezaji soka watatu wanaotajwa kuwa matajiri kwa nchi ya Nigeria.
Hadi kufikia mwaka June 2017 hii ndio ilikuwa list ya wachezaji watatu matajiri katika nchi ya Nigeria, haijawekwa wazi kwa nini John Obi Mikel amekosekana katika list hii, licha ya kuwa wengi wanaamini kuwa ni mchezaji tajiri pia.
1- Odion Ighalo alizaliwa mwaka 1989 Lagos Nigeria na alianza kucheza soka katika club ya Prime FC, amecheza vilabu mbalimbali kama Udenise ya Italia, Granada FC na Watford ya England kabla ya mwanzo mwa mwaka 2017 kuamua kujiunga na Changchun Yatai F.C ya China, Ighalo analipwa mshahara wa dola 250000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 550 za kitanzania.
2- Ahmed Musa tukiachana na Ighalo kuna staa mwingine ambaye ana umri wa miaka 24 Ahmed Musa ambaye kwa sasa anaichezea club ya Leicester City ya England, thamani yake kama mchezaji ni dola milioni 20 wakati Ighalo thamani yake ni dola milioni 11, Ahmed Musa amezidiwa mshahara na Ighalo yeye analipwa dola 77000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 170 kwa wiki.
3- Obafemi Martins amezaliwa 1984 lakini aliondoka kwao Nigeria kwenda kuanza maisha ya soka akiwa na umri wa miaka 16, Obafemi amecheza vilabu mbalimbali Ulaya kama Inter-Milan ya Italia, Newcastle United ya England, Birmingham City ya England, Vfl Wolfsborg.
Utajiri wa Obafemi haujaishia katika mshahara wa dola milioni 1.6 kwa mwaka anaolipwa na Seattle Sounders ya Marekani bali anamiliki magari ya kifahari kama Lamborghini, Porsche Gemballa na Ferrari na anamiliki hoteli zaidi ya moja Italia.
SOURCE: Naija.ng
Rekodi aliyoiweka Guardiola baada ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwezi