Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya Dar es Salaam Young Africans leo Jumamosi ya January 27 2018 walikuwa katika uwanja wa Azam Complex, Mbande Chamazi kucheza game yake ya 15 Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya wenyeji wao Azam FC.
Yanga na Azam FC ndio walikuwa wanakutana katika mchezo wa Ligi katika uwanja wa Chamazi kwa mara ya kwanza lakini huo ulikuwa ni mchezo wa 32 kwa timu zote mbili kuwahi kukutana na mchezo wa 19 katika Ligi Kuu kwa timu hizo kukutana.
Azam FC katika michezo ya Ligi Kuu wamewahi kuifunga Yanga mara 5, sare 7 na kupoteza mara 6, kwa mashindano yote Azam FC kashinda mara 11, sare 8 na kupoteza michezo 13 ikiwemo mchezo wao wa leo baada ya kuruhusu kufungwa kwa magoli 2-1 dhidi ya Yanga.
Magoli ya Yanga yalifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 31 na Gadiel Michael dakika ya 44 wakati goli pekee la Azam FC lilifungwa mapema tu dakika ya 4 kupitia kwa Shaban Iddi Chilunda, ushindi huo unaifanya Yanga kuendelea kusalia nafasi ya tatu kwa kufikisha point 28 na Azam FC wakibaki nafasi ya pili kwa kubaki na point zao 30.
PICHA HISANI YA AZAM TV
Alichokiandika Jerson Tegete baada ya Nyosso kumpiga shabiki