Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete licha ya kuwa sasa amewekeza nguvu kubwa katika kuhakikisha jimbo lake la Chalinze linapata maji kila kijiji, ameendelea kuhakikisha jamii ya wafugaji wanapata elimu bora ya ufugaji pasipo kuharibu ardhi.
Ridhiwani Kikwete ambaye awali maafisa mifugo wa halmashauri ya Chalinze walikuwa wanashindwa kufika baadhi ya maeneo kutokana na kukosa usafiri, amewakabidhi pikipiki August 21 kuhakikisha kila mmoja anatekeleza kazi yake pasipokuwa na kisingizio.
Pikipiki 10 aina ya Sanlg August 21 zimekabidhiwa kwa maafisa mifugo wa halmashauri ya Chalinze kwa ajili ya kuhakikisha wanafika kila kona, kutoa elimu ya ufugaji bora na kisasa, pasipo kuharibu mazingira, kwa mujibu wa sensa ya mifugo ya mwaka 2012 halmashauri ya Chalinze ina jumla ya ng’ombe 240,000, mbuzi 94,000, kondoo 54,000 na kuku 380,000.
Zaidi tazama Mbunge Ridhiwani Kikwete alivyokabidhi pikipiki hizo hapa
VIDEO: Mfumo utaokaofuatilia mwenendo wa mabasi ya abiria popote litakapokuwa