Robo fainali ya tatu ya michuano ya mataifa ya Ulaya 2016 imechezwa usiku wa July 2 2016 kwa kuzikutanisha timu za taifa za Ujerumani dhidi ya timu ya taifa ya Italia, huu ni mchezo ambao mashabiki wa soka kwa kiasi kikubwa walikuwa wanautabiria ndio mchezo utakaotoa Bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2016.
Rekodi za timu hizo mbili zilikuwa zinaonekana kuwa nzuri kwa Italia kuliko Ujerumani, kitu ambacho hakikuisaidia Italia kupata matokeo, kabla ya mchezo wa leo Italia alikuwa kamfunga Ujerumani mara 15 katika michezo 34 waliowahi kucheza, sare mara 11 na kupoteza mara 8, bahati ilionekana kutokuwa nzuri kwa Italia baada ya kukubali kipigo cha mikwaju ya penati 6-5.
Hatua ya mikwaju ya penati ilikuja baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya goli 1-1, magoli ambayo yalifungwa na Mesut Ozil kwa Ujerumani dakika ya 65, lakini Italia walikuja kuchomoa goli hilo dakika ya 78 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Leonardo Bonucci. Kwa matokeo hayo Ujerumani itakutana na mshindi kati ya Ufaransa na Iceland katika hatua ya nusu fainali.
#Germany imefanikiwa kuitoa #Italy kwa mikwaju ya penati. pic.twitter.com/kwHXeLS8jd
— millard ayo (@millardayo) July 2, 2016
Mikwaju ya penati iliyoitoa Italia dhidi ya Ujerumani pic.twitter.com/uky6kfHudz
— millard ayo (@millardayo) July 2, 2016
GOLI LA MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE