Usiku wa February 16 2017 ilikuwa ni siku ya kihistoria tena kwa mtanzania Mbwana Samatta ambapo akiwa na KRC Genk alipata nafasi ya kucheza mchezo wa 32 bora wa Europa League ugenini dhidi ya FC Astra ya Romania hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza hatua hiyo.
Katika mchezo huo uliyochezwa Romania, KRC Genk wakiwa ugenini wamefanikiwa kupata sare ya kufungana goli 2-2, huku Mbwana Samatta akihusika katika upatikanaji wa goli la pili la Genk lililofungwa na Leandro Trossard dakika ya 83 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Siebe Schrijvers.
Goli la kwanza la KRC Genk lilifungwa na Timoty Castagne dakika ya 25 lakini FC Astra walisawazisha goli hilo dakika ya 43 kupitia kwa Constantin Budescu na dakika ya 90 Takayuki Seto akainusuru FC Astra kwa kuisawazishia goli, Genk sasa watacheza mchezo wa marudiano na FC Astra katika uwanja wao wa Luminus Arena nchini Ubelgiji.
FULL HD: All goals N’gaya vs Yanga February 12 2017, Full Time 1-5