Kuelekea kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu England na kuelekea kipindi cha usajili cha majira ya joto, tayari majina ya wachezaji wanaonekana kufanya vizuri yameanza kuhusishwa kujiunga na timu fulani, Wilfred Ndidi ambaye alijiunga na Leicester City January akitokea KRC Genk ya Ubelgiji jina lake limerudi kwenye headlines za usajili tena.
Ndidi ambaye ana miezi michache toka ajiunge na Leicester City akitajwa kama mbadala sahihi wa kiungo N’golo Kante aliyejiunga na Chelsea, ameanza kuripotiwa kuhitajika na timu za Arsenal na Man United, mtandao wa 90min.com umeripoti timu hizo kuanza kumfuatilia kwa karibu kutokana na kiwango chake.
Wilfred Ndidi ni miongoni mwa wachezaji wa zamani wa KRC Genk waliyompokea Samatta wakati anajiunga na timu hiyo mwaka 2016, kutokana na Ndidi kutokea Nigeria, Omar Colley kutoka Gambia na Samatta kutokea Tanzania wameonekana mara kadhaa kuwa karibu hiyo inatokana na wote kutokea Afrika.
ALL GOALS: Taifa Stars vs Botswana March 25 2017, Full Time 2-0