Kocha wa club ya Everton ya England Ronald Koeman leo September 6 2017 ameripotiwa kumuita nahodha wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya England anayeichezea Everton kwa sasa Wayne Rooney na kuongea nae kuhusu tuhuma zinazomkabili za kuendesha gari akiwa amelewa.
Rooney anatuhumiwa na Polisi wa Cheshire baada ya kukamatwa usiku wa Ijumaa ya August 31 2017 akiwa anaendesha gari akiwa amelewa, kitu ambacho ni kinyume na sheria, baada ya kukamatwa Rooney aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa mahakamani September 18 2017.
Staa huyo wa zamani wa Man United kama akikutwa na hatia kwa kosa hilo club ya Everton itamkata mshahara wa wiki mbili unaokadiriwa kufikia pound 320000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 900, Rooney hata hivyo amepewa onyo baada ya kuzungumza kwa muda mrefu na kocha Ronald na kuambiwa kama anataka kudumu katika club hyo anabidi abadilike.
CHANZO: express.co.uk
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0