Suala la michoro mwilini ama Tattoo kama inavyofahamika na wengi sasa limekuwa kama sehemu ya utamaduni katika Ulimwengu wa soka ambapo siku hizi ni rahisi sana kuwaona wachezaji wakiwa na michoro mingi katika miili yao.
Hapa ninayo list ya wachezaji wa soka 20 ambao wanatajwa kuwa vinara wa tattoo duniani huku mingi kati ya tattoo hizo zikiwakilisha mambo mbalimbali kwa wahusika.
Hii ni Top 20 ya Wachezaji wanaotajwa kuongoza kwa kuwa na Tattoo
20: Aleksandar Kolarov
Aleksandar Kolarov ni mchezaji wa Serbia anayekipiga Manchester City ni miongoni mwa wenye tattoo huku moja ya tattoo zake ikisomeka The Koi fish ikiwa ni alama ya bahati na heri.
19: Mauro Icardi
Nyota wa Internazionale Milan Mauro Icardi ameonesha tattoo mpya ya simba ikiwa na majina ya mabinti wake Francesca na Isabella.
18: Memphis Depay
Memphis Depay anatajwa kuwa ni mpenzi wa tattoo. Memphis Depay alisaini kuichezea Olympique Lyonnais akitokea Manchester United na licha ya kuwa anafanya vizuri amekuwa anachora tattoo mara kwa mara na moja kati hizo ni maneno “Dream Chaser”, pia ana mchoro mkono wa kushoto ambao ni heshima ya babu yake pamoja na mchoro wa simba mgongoni na tattoo nyingine maarufu ni ile ya kwenye mdomo ambayo inasomeka ‘succesvol’ ikiwa na maana ya mafanikio.
17: Tim Cahill
Kiungo wa Australia na Hangzhou Greentown FC naye ametajwa katika list hii. Cahill alicheza miaka saba katika klabu ya Millwall kabla ya kujiunga Everton alikodumu kwa miaka mitano sasa.
16: Sergio Ramos
Mlinzi na nahodha wa Real Madrid anatajwa kuwa mmoja kati ya walinzi wenye tattoo nyingin duniani. Sergio Ramos ana tattoo zenye maana nyingi: majina ya wazazi wake “JM” na “P” aliyoyaandika kuizunguka namba “7”, ambayo ndiyo aipendayo. Pembeni ya tattoo hii kuna maneno, “I’ll never forget you” ambayo ni maalumu kwa wazazi wake. Pia Ramos ana maneno mengine, “Lies in the memory of those alive” yakiambatana na tarehe 9/11 na 3/11 kukumbuka matukio ya kigaidi New York na Madrid. Chini ya maneno hayo ana nyota ya David ikiwa kumbukumbu ya Antonio Puerta.
15: Marco Materazzi
Mlinzi wa zamani wa Inter Milan, Marco Materazzi, anakumbukwa kwa tukio lake la kupigwa kichwa na Zinedine Zidane na ana michoro ya mataji yote aliyowahi kushinda kuanzia World Cup, Serie A, Italian Cup na UEFA Champions League.
14: Kevin Prince Boateng
Boateng ni kati ya wachezaji waliopita kwenye timu nyingi kwa sasa anakipiga UD Las Palmas kwenye La Liga na anaingia katika list hii baada ya kuchora ramani ya nchi yake ya Ghana na jina la nchi katika mkono wake. Pia kuzunguka mbavu zake kuna maneno ya Kichina yanayosomeka kwa Kiswahili ukoo, afya, mapenzi, mafanikio na uaminifu na michoro mingine sehemu ya juu ya mwili.
13: Ezequiel Lavezzi
Licha ya kuwa mshambuliaji tegemezi wa Argentina pia ni kinara wa tattoo duniani. Hakuna shaka kwamba sasa ametimkia kwenye ligi ya China na kumfanya ndiye mchezaji anayeoongoza kwa tattoo kwenye ligi hiyo. Ezequiel Lavezzi ni Mkatoliki ndiyo maana kifuani pake ana mchoro wa Yesu na tattoo ya Bikira Maria katika mkono wa kulia na mchoro mwingine unaonekana mgongoni.
12: Daniel Alves
Daniel Alves miongoni mwa tattoo zake ni picha ya mkewe katika mkono wa kulia na jina la mtoto wake wa kiume kuzunguka kifua.
11: Zlatan Ibrahimovic
Huyu jamaa ana tattoo 50 za kujitolea ambapo wakati wa mchezo wa Ligue 1 February 16, 2015, PSG vs Caen, Zlatan Ibrahimovic alionesha tattoo 50 za muda ambapo kila tattoo iliwakilisha jina moja kati ya majina ya watu 805m wenye njaa duniani.
10: David Beckham
Miongoni mwa tattoo maarufu katika mwili wa staa huyu wa zamani wa Manchester United ni majina ya wana familia yake. David Beckham alikuwa na jumla ya tattoo 32 ambapo miongoni mwake ni majina wa watoto wake Romeo, Cruz na Brooklyn, na jina la mkewe Victoria. Tattoo nyingine ni Aya ya Biblia iliyoandikwa kwa lugha ya Hebrew.
9: Stephen Ireland
Lengo la Stephen Ireland ni kuhakikisha mgongo wake unafunikwa na tattoo ya mbawa, huku pia akiwa na tattoo nyingine mkononi. Wapo wachezaji wana tattoo zinazotatanisha mmoja kati yao ni Stephen Ireland.
8: Martin Skrtel
Martin Skrtel ni mmoja kati ya walinzi wa kihistoria katika klabu ya Liverpool aliyodumu nayo kwa misimu 9 na sasa anakipiga Fenerbahçe. Licha ya kuwa ni mmoja kati ya walinzi bora pia anaingia kwenye list hii akijulikana kuwa mmoja kati ya wanasoka wenye michoro mingi.
7: Nigel de Jong
Nigel de Jong ni mmoja pia katika wanamichezo wenye tattoo za kutosha mwilini. De Jong bado anaendelea kuchora tattoo na amekuwa akiweka wazi kila anapofanya hivyo kwa kupost picha kwenye Instagram au Facebook.
6: Tim Howard
Huyu anatajwa kuwa mlinda mlango mwenye tattoo nyingi zaidi duniani akiichezea Everton na timu ya Taifa la Marekani. Kati ya michoro aliyo nayo ni pamoja na sura za watoto wake alizochora kifuani. Pia ana mchoro wa namba yake 24 katika mbavu na moja kati ya michoro maarufu ni pamoja na namba za kirumi MCMLXXIX MMVII MMV ambazo ni 1979 2007 2005.
5: Raul Meireles
Raul José Trindade Meireles alicheza katika klabu za Boavista, Porto, Liverpool, Chelsea, na baadaye Fenerbahçe, kabla ya kustaafu. Raul Meireles ni mpenzi wa tattoo tangu akiwa na miaka 18. Katika mwili wake kuna michoro mbalimbali ikiwemo ya picha ya mkewe na binti yake.
4: Daniel Agger
Daniel Munthe Agger ni mlinzi na nahodha wa zamani wa Denmark ambapo mara ya mwisho aliichezea Brøndby IF huku akicheza misimu 9 akiwa na Liverpool sambamba na Martin Skrtel ambapo waliunda pair ya walinzi wenye tattoo nyingi zaidi kwenye Premier League. Jambo lingine kubwa kwake na kwamba naye ni mchoraji aliyefuzu kuchora tattoo. Moja ya tattoo anayokumbuka nayo ni aliyochora August 2012 ikiwa ni herufi “YNWA” kwenye kidole cha mkono wa kulia akimaanisha “You’ll Never Walk Alone”.
3: Djibril Cisse
Huyu licha ya kuwa mchezaji hodari zama zake pia ni mwigizaji na DJ. Djibril Cisse ametembelea nchi kadhaa duniani wakati akicheza soka. Mbali na mitindo kadhaa ya nywele Djibril Cisse tattoo ni miongoni mwa vitu vinavyomtambulisha zaidi.
2: Gregory Van der Wiel
Gregory Van der Wiel winga wa kushoto wa kihistoria wa Paris Saint Germain ambaye sasa anakipiga Fenerbahçe. Hivi karibuni Van der Wiel aliongeza tattoo ya Pharaoh kwenye mwili wake ambapo ni nyongeza ya tattoo zilizopo mikononi, kifuani na mgongoni. Mwaka 2014 Van der Wiel aliingia kwenye mabishano ya mzaha na FIFA14 (EA Sports video game) baada ya kuonekana bila kuwa na tattoo zake.
1: Jermaine Jones
Jermaine Junior Jones ni mwanasoka wa Marekani ambaye hucheza nafasi ya kiungo wa ulinzi kwenye timu ya Taifa la Marekani. Awali amezichezea klabu za Eintracht Frankfurt, Bayer Leverkusen, Blackburn Rovers, Schalke 04, Beşiktaş, na New England Revolution.
MAAJABU?!! TUMBO LIMETOBOLEWA LAKINI ANATEMBEA!!!