Timu ya taifa ya Argentina inatajwa kuwa katika nafasi mbaya ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi, hiyo inatokana na Argentina kuwa nafasi ya tano katika msimamo wenye timu 10 huku timu nne za juu ndio zitafuzu.
Kufuatia Argentina kuvuna point mbili katika mechi zao tatu zilizopita, mjadala kutoka katika moja ya vituo vya TV Argentina umetoa madai tofauti kutokana na urafiki wa Lionel Messi na kocha wa timu yao ya taifa ambao umetajwa kuwa Messi amemshawishi kocha asimuite Mauro Icardi kikosini licha ya kuonesha uwezo mkubwa akiwa na Inter Milan.
Urafiki wa karibu wa Messi na mchezaji mwenzake wa zamani wa FC Barcelona Maxi Lopez ambaye ana ugomvi na Mauro Icardi kutokana na kuwa alimpokonywa mke, hivyo Messi anatajwa kutovutiwa na kitendo hicho na kumshawishi kocha asimuite Icardi, Mauro Icardi ameichezea Argentina kwa dakika 8 tu, hivyo wengi walitamani kumuona akiongeza nguvu.
ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1