Kuelekea mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliyopo katika kalenda ya FIFA wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya Botswana September 2 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, wachezaji wa kimataifa wa Tanzania walioitwa wengi tayari wameungana na wenzao.
Miongoni mwa wachezaji waliyoitwa Taifa Stars ni Simon Msuva anayecheza Difaa El Jadid ya Morocco na Farid Musa anayecheza Tenerife ya Hispania lakini vipi mbona hatuwaoni na wenzao, ukilinganisha wenzao wa nje Abdi Banda, Mbwana Samatta na Elias Maguli wameshawasili?
Kocha mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga amezungumzia kuhusiana na ishu hiyo “Namshukuru Mungu vijana wako salama lakini kuna wachezaji wawili bado hawajafika, Msuva alikuwa na tatizo la visa ilikwisha kule, hivyo tulilazimika kubadilisha mara tatu tiketi yake kule, lakini hadi saa tano asubuhi leo kulikuwa na uwezekano wa kuanza safari”
“Kuhusu Farid tayari yupo kambini amefika jioni hii lakini amepumzika kutokana na safari ndefu lakini Monreal anayecheza Ureno ndio tunadhani mtu pekee ambaye hatohudhuria mechi hii, kwa kiasi kikubwa asilimia 90 wachezaji wote wapo”
Video ya dakika 2 ikionyesha Hat-Trick ya Okwi iliyookoa Milioni 5