Ikiwa zimepita siku 2 toka serikali kupitia kwa waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Nape Moses Nnauye kutangaza kuufungia uwanja wa Taifa Dar es Salaam kutumia kwa vilabu vya Simba na Yanga, leo October 4 2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans imetangaza kuomba uwanja mbadala watakaotumia kuchezea mechi zao.
Yanga kupitia barua waliyoitoa leo iliyoandikwa na katibu mkuu wao imeomba kuutumia uwanja wa Amaan Zanzibar kama uwanja wao wa nyumbani, katika kipindi hiki ambacho wamezuiwa kutumia uwanja wa Taifa.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri waziri Nape alitangaza maamuzi ya kuzizuia timu za Simba na Yanga kwa muda usiojulikana kuutumia uwanja wa Taifa Dar es Salaam kutokana na vurugu na uharibifu uliotokea siku ya mchezo wao wa watani wa jadi uliomalizika kwa sare ya goli 1-1, ila mashabiki walivunja viti na wengine mageti ya kuingilia.
Baada ya waziri Nape kuzuia Yanga na Simba kutumia uwanja wa Taifa, Yanga imeomba kutumia uwanja wa Amaan Zanzibar kama uwanja wa nyumbani. pic.twitter.com/x7NV63e687
— millard ayo (@millardayo) October 4, 2016
ULIPITWA NA MAAMUZI YA WAZIRI NAPE KUHUSU YANGA NA SIMBA? TAZAMA HAPA