Septemba 25 2016 ilikuwa ni siku ambayo wabunge wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walicheza mchezo wa hisani kwa ajili ya kukusanya fedha za watu waliopata na tetemeko la maafa Bukoba, wabunge walijigawa katika timu mbili wale wabunge ambao wanaishangilia Yanga na wabunge wa Simba.
Mashabiki ambao walikuwa wamejitokeza uwanjani kuangalia wabunge hao wakiwa katika mavazi ya timu wanazozishabikiwa mbunge na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba alikuwa ni miongoni mwa wabunge waliowanyanyasa wabunge wa Simba kwa kuwaonesha uwezo mkubwa katika kuuchezea na kumiliki mpira.
Hata hivyo katika mchezo huo ambao waziri Mwigulu aliifungia magoli mawili timu ya timu ya wabunge wa Yanga kati ya ushindi wa goli 5-2, waziri Mwigulu alionekana kuwasumbua baadhi ya wabunge kwa kupiga chenga, hadi dakika 90 zinamalizika wabunge wa Yanga waliondoka na ushindi wa goli 5-2.
Magoli ya wabunge wa Yanga yalifungwa na Jadal Hamisi dakika ya 4, Musa Sima dakika ya 5, Hamidu Bolali dakika ya 9 na mwisho Mwigulu Nchemba akahitimisha kwa kufunga magoli mawili ya mwisho na kuwafanya wabunge wa Yanga kuondoka na Kombe la Ubingwa wa mchezo huo wa Hisani.
GOALS: TP Mazembe vs Yanga August 23 2016, Full Time 3-1