Shirikisho la soka barani Afrika CAF leo Jumatano ya December 13 2017 limetangaza ratiba ya michuano ya club Bingwa Afrika na michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika CAF msimu wa 2017/2018.
Ratiba hiyo imepangwa baada ya kuchezeshwa droo na Tanzania tuna wawakilishi wawili ambao ni club ya Yanga ambayo itacheza Kombe la club Bingwa Afrika na club ya Simba ambayo itacheza Kombe la shirikisho barani Afrika CAF.
Yanga wamepangwa kucheza dhidi ya St Louis ya visiwa vya Seychelles katika round ya kwanza na wakipita watacheza na mshindi kati ya Al Merreikh ya Sudan vs Township ya Botswana.
Simba wao ambao watakuwa wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la shirikisho watacheza dhidi ya Gendarmerie Tnale ya Djibout katika round ya kwanza na wakipita watacheza na mshindi kati ya Al Masry ya Misri vs Green Buffalos ya Zambia.
VIDEO: Atayofanya Mo Dewji kwa Simba ndani ya mwaka mmoja