Timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes imefanikiwa kuwashangaza wengi katika michuano ya Kombe la CECAFA nchini Kenya baada ya kufanikiwa kuwatoa mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo timu ya taifa ya Uganda The Cranes.
Zanzibar imefanikiwa kuitoa Uganda katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo kwa kuifunga jumla ya magoli 2-1, hivyo ushindi huo unaifanya Zanzibar Heroes ikutane na Kenya katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo.
Zanzibar imefanya vizuri kuliko Tanzania bara ambayo imeondolewa katika michuano hiyo kwa kupoteza game tatu na kutoka sare game mmoja pekee ya hatua ya makundi, hivyo Zanzibar ndio muwakilishi pekee wa Tanzania aliyesalia katika michuano hiyo.
Baada ya Zanzibar kufuzu Rais mstaa wa awamu ya nne Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza kwa kuandika maneno haya
“Nawapongeza Zanzibar Heroes kwa kututoa kimasomaso na kutinga fainali. Nawatakia kila la kheri katika mechi ya fainali waibuke na kombe na watupe raha ambayo Watanzania tumeikosa kwa muda mrefu”
Kwa upande wa mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe aliipongeza Zanzibar na kuomba ZFA awe mwanachama wa FIFA na TFF ipumzike kidogo ili wajipange upya
“Kama hatutaki Zanzibar kuwa Mwanachama wa FIFA kama ilivyo Scotland. Tuseme kwa miaka 5 ijayo kuanzia mwaka huu ZFA ndio mwanachama FIFA na CAF ili TFF ipate muda wa kujipanga. Ndani ya hiyo miaka 5 nawaambia Zanzibar itakwenda AFCON na hata Kombe la Dunia.#MsemaKweliMpenziWaMungu“
UTANI: Haji Manara kwa wapinzani wao Yanga baada ya Simba kumpata MO Dewji