Uzalendo Kwanza walifanikiwa kufika Handeni ikiwa ni siku moja imepita toka watoke Tanga Mjini kutoa msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya zaidi ya Tsh Milioni 29, wamepata bahati kwa DC Gondwe ambaye ameamua kuwapa shamba la hekari 130.
Baada ya Uzalendo Kwanza kupewa hekari 130 mwenyekiti wao Steven Nyerere alizungumza mbele ya DC Gondwe “Tanzania inatudai sisi lakini sisi hatuidai Tanzania kitu cha kwanza inachotudai sisi ni amani, amani inatudai sana na bado tunaingalia hii amani inalegalega”>>> S.Nyerere
DC Gondwe katoa hekari 130 kwa Uzalendo Kwanza, zinauwezo wa kuzalisha nanasi bora zaidi ya USA