Idara ya uhamiaji leo December 21 2016 ilitoa tamko kwa vilabu vyote vya Ligi Kuu Tanzania bara kutoendelea kuwatumia wachezaji wake wa kigeni hadi watakapotimiza masharti ya uwepo wao nchini kisheria.
Uhamiaji wamevitaka vilabu vya Simba, Yanga na Azam FC kuhakikisha wachezaji wake na makocha wao wa kigeni wanapata vibali vya kufanyia kazi nchini pamoja na kuishi, hata hivyo Yanga wao wachezaji wao wana vibali vya kazi na vya kuishi nchini isipokuwa makocha wao ndio wana vibali vya kazi pekee.
Kwa upande wa watani zao wa jadi Simba wao hawajatimiza vigezo hivyo kwa wachezaji wao wa kigeni na makocha wao, hivyo hawaruhusiwi kuendelea kuwatumia wachezaji wao ambao hawana vibali mpaka watakapo vipata vibali.
ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3