Viongozi wa Shirikisho la soka Afrika CAF wakiongozwa na Rais wa shirikisho hilo Ahmad Ahmad wamefanya mabadiliko ya baadhi ya sheria za uendeshaji soka Afrika, kwa ajili ya kufanya uboreshaji zaidi wa soka katika nchi za Afrika.
CAF wametangaza kuzifanyia mabadiliko baadhi ya sheria, maamuzi ambayo yameafikiwa katika mkutano wao uliyofanyika Casablanca Morocco.
1- Zamani marefa walikuwa wanalipwa na vyama vya ndani ya nchi husika wanapokwenda kuchezesha game lakini kwa sasa imekuwa tofauti, malipo ya michuano inayoratibiwa na CAF marefa watalipwa na CAF.
2- CAF pia wamebadilisha michuano ya mataifa ya Afrika itakuwa inachezwa mwezi June na sio January kama ilivyokuwa sababu zikidaiwa kuwa ni kutotaka kuharibu ratiba za wachezaji wanaocheza soka Ulaya.
3- Mechi za michuano ya Club Bingwa Afrika na Kombe la Shirkisho la Afrika game zake zitakuwa zinachezwa katikati ya wiki kama ilivyo kwa michuano ya Club Bingwa Ulaya na Europa League na weekend itakuwa ni mechi za Ligi tu.
4- CAF pia wamefanya mabadiliko ya kuanza kwa Ligi zote za soka Afrika zitatakiwa ziwezinaanza August na kumalizika May na sio kama inavyofanyika sasa baadhi ya nchi Ligi zake haziendani na nchi nyingine za Afrika.
Rekodi aliyoiweka Guardiola baada ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwezi