Zipo tabia ambazo huenda hukudhani kuwa ni kero hasa unapokuwa sehemu za kujipatia huduma za chakula hasa Mgahawani na Hotelini lakini Wadau wa Afya duniani wanashauri na kuonya baadhi ya tabia ambazo hujitokeza mara kwa mara lakini sio nzuri na huweza kukera watu.
1. Kupiga vidole kama ishara ya kumuita mhudumu
Hii ni pale ambapo mtu huamua kuwasiliana na mhudumu wa eneo hilo kwa ishara ikiwa ni pamoja na kumuita kwa ajili ya huduma kwa kutumia vidole au kuwapigia mluzi. Tabia hii inatafsiriwa kuwa ya kuudhi na dharau na kwamba ni vyema kumuita mhudumu kwa kutumia neno ‘mhudumu’.
2. Kuongea wakati chakula kimejaa mdomoni
Watu wengi pia hutumia muda wa kula kupiga stori mbalimbali. Inaweza kuwa sio tatizo lakini tatizo huja pale ambapo mtu hulazimisha kuongea wakati chakula kimejaa mdomoni. Suala hili hueza kusababisha kinyaa kwa watu aliokaa nao au hata walio karibu naye.
3. Kulamba mikono
Wapo wengine pia hupenda kula chakula kwa kutumia mkono jambo ambalo halina shida. Shida ya ulaji huu inaanzia pale mtu anapoanza kula na kulamba vidole au hata mkono mzima na wakati mwingine akitoa sauti ambazo sio nzuri hata kuweza kusababisha kinyaa na kukereka.
4. Kupiga picha kwa ajili ya mitandao ya kijamii
Suala hili mara nyingi hufanywa na wasichana ambao hupenda sana kupiga picha na kuchukua video ili tu kuzipost kwenye mitandao ya kijamii. Mara nyingi zoezi hili huwafanya wachukue muda mwingi ili wahakikishe wamepiga picha na kuchukua video nzuri za tukio hilo la chakula. Hii imetajwa kuwa tabia mbaya ya wakati wa kula.
5. Kufutia mikono kwenye vitambaa vya mezani
Hili nalo ni jambo linaloshangaza pale ambapo mtu anamaliza kuna chakula na kuamua kujifutia mikono kwa vitambaa hivyo vya mezani. Ni vyema baada ya kula mtu kunyanyuka na kunawa kwenye bomba au sehemu iliyowekwa maji ya kunawa badala ya kutumia vitambaa hivyo.
6. Kuchanganya vinywaji tofauti kwenye glasi moja
Wapo pia wenye tabia ya kuchanganya vinywaji tofauti tofauti kwenye glasi moja. Suala hili pia limetajwa kuwa sio la kistaarabu, ni vyema mtu kuomba glasi nyingine ile kuzitumia kwa vinywaji hivyo na sio kuvichanganya.
7. Kupenga makamasi
Inawezekana hili limezidi mambo yote pale ambapo mtu anaamua kupenga makamasi katika eneo hilo hilo ambalo watu wanakula. Ni vyema kutoka nje au kutakuta ilipo bafu au choo ili kumaliza haja hiyo ili kuepusha kukera watu walioko eneo hilo.
Show ya Alikiba kwenye One Africa Music Festival, New York…itazame hapa!!!