Asubuhi ya August 17 2017 taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana jengo la club ya Dar es Salaam Young Africans la Jangwani kuhusishwa kuwa litapigwa mnada Jumamosi ya August 19 kwa madai ya kudaiwa malimbikizo ya kodi ya ardhi inayofikia Tsh milioni 300.
Katibu Mkuu wa Dar es Salaam Young Africans Charles Boniface Mkwasa amezungumzia ishu hiyo na kukiri kuwa ni kweli Yanga wanadaiwa lakini hawana uwezo wa kuilipa hela hiyo kwa mara moja.
“Tumeandika barua wizarani ya kupata kibali cha kuondoa au kupunguza riba ili tuweze kulipa lakini bado inaonekana mawakala hawa ambao wamepewa jukumu kukusanya mapato ya serikali wanadai kwa sababu wanapata asilimia 10 ya kukusanya” >>> Mkwasa
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0