Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Jumapili ya November 12 2017 ilikuwa nchini Benin kucheza mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao Benin, mchezo ambao unatumika katika kupanga viwango vya FIFA vya kila mwezi.
Taifa Stars ikiwa ugenini ilikuwa inacheza na Benin ambao wapo nafasi ya 79 katika viwango vya soka kwa ubora duniani ukilinganisha na Tanzania ambao wapo nafasi ya 136 katika viwango vya FIFA, hivyo kutoka sare ya 1-1 leo dhidi ya Benin inatoa nafasi nzuri kwa Stars kupanda viwango vya FIFA.
Mchezo dhidi ya Benin unakuwa ni mchezo wa 14 wa Taifa Stars kucheza wakiwa chini ya kocha wao Salum Mayanga lakini unakuwa ni mchezo wa saba kwa Taifa Stars kupata sare wakiwa chini ya Mayanga na wameshinda game 6 na kupoteza mchezo mmoja pekee dhidi ya Zambia katika michuano ya COSAFA.
Taifa Stars wakiwa katika uwanja wa Stade d’Amitie leo dhidi ya Benin walianza kuruhusu goli kwa mkwaju wa penati dakika ya 30, penati ambayo imepatikana kwa utata na kupigwa na Stephano Sessegnon lakini Elias Maguli aliisawazishia Taifa Stars dakika ya 51 kwa pasi nzuri kutoka kwa Shiza Kichuya.
Taarifa rasmi kutoka Ubelgiji, Samatta atafanyiwa upasuaji