Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta leo August 31 2017 katika mazoezi ya Taifa Stars ameshindwa kumaliza mazoezi baada ya kuumia eneo la kisigino cha mguu wa kushoto.
Baada ya mazoezi tumempata daktari wa viungo wa Taifa Stars Gilbert Kigadya, vipi shida nini kwa Samatta? kwenye mechi dhidi ya Botswana September 2 2017 uwanja wa Uhuru atakuwepo.
“Samatta tatizo lake dogo tu ameugonga mguu wakati anarudisha baada ya kuokoa wakati anaushusha mguu ukagonga chini kwa hiyo ni maumivu ya kawaida na uhakika kesho atakuwa vizuri tu”>>> Gilbert
Samatta kaipata ofa ya kumrithi Van Persie? ukimuuliza atakujibu hivi