June 30, 2017 katika story zilizopewa uzito mkubwa ni pamoja na issue inayo-make headlines ya Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CHADEMA, Edward Lowassa kuitwa na CDI lakini akaambiwa upelelezi haujakamilika.
Story hiyo na nyingi zimeruka kwenye Televisheni, Magazeti, Randio na mitandao mbalimbali na kama ulizikosa kuitia vyombo hivyo nimekukusanyia na kukusogezea hapa kupitia millardayo.com.
Taasisi ya APEC imezindua kampeni maalum "Usiue Askari Wetu, Mlinde" kufuatia mauaji ya Askari na raia yanayotokea Mkoa wa Pwani. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Halmashauri zilizopokea walimu wapya wa Sayansi, Hisabati na wataalamu wa Maabara zimetakiwa kuwapa stahiki zao ndani ya siku 7. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha viwanda vya kubangua na kusindika korosho katika Wilaya za Mkuranga, Mtwara na Tunduru. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Imeelezwa kuwa Watanzania 1,009 ambao walikuwa nguvukazi ya Taifa wamefungwa maisha kwenye magereza mbalimbali nje ya nchi. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Serikali inaendelea kutoa vibali vya kuajiri watumishi wengine ili kuziba nafasi za walioondolewa kutokana na kuwa na vyeti feki. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Mkazi mmoja wa Nyashana, Mwanza Sangija George (27) ameuawa kwa kuchomwa kisu shingoni wakati akimuokoa dada yake asibakwe. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Wabunge watatu wa CHADEMA wamefungua kesi Mahakamani kupinga adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge kwa kukiuka maadili na kanuni #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
CHADEMA imesema kuwa kauli aliyoitoa Lowassa kuhusu Masheikh wa UAMSHO ni msimamo wa chama na itaendelea kupigania haki zao. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Mkazi wa Sumbawanga, mkoani Rukwa Fokas Pera (48) ameuawa kwa kucharangwa mapanga kichwani na rafiki yake kwa deni la mbao 2. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
RC Arusha Mrisho Gambo anadaiwa kumfukuza DC Arumeru ktk kikao cha kujadili hoja za Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
"Ni aibu kwetu hatuwezi kuwa na watendaji wanaoendekeza rushwa, tutawanyoosha." – Prof. Makame Mbarawa. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Mashtaka 28 yakiwemo ya kughushi na kutakatisha fedha $375,418 yanawakabili Rais wa TFF, Katibu Mkuu wa TFF na Mhasibu wa TFF. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani anatarajia kukutana na Maafisa wa juu wa Jeshi la Polisi kuzungumzia matukio ya mauaji Mkoani Pwani. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Baadhi ya wanaCCM Kibiti na Rufiji wameutaka uongozi wa CCM Taifa kuangalia namna ya kuahirisha uchaguzi wa chama kwenye Wilaya hizo. #UHURU
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Makampuni 25 yanatarajia kushushiwa mabango yake ya matangazo baada ya kushindwa kuilipa Manispaa ya Ubungo kodi ya Tsh. 648m. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma amewataka mawakili wapya kutenda haki akiwaasa kutokuwa mawakala wa rushwa Mahakamani. #UHURU
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Baraza la Wazee wa CHADEMA limelaani kauli ya Mzee Mwinyi kuliandaa Taifa kisaikolojia kwa kutamani Rais JPM aongoze milele. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Wabunge wameipinga Serikali kupeleka Bungeni miswada ya marekebisho ya sheria za gesi, mafuta na madini kwa hati ya dharura. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Waziri Mkuu wa zamani Lowassa anaamini alichokisema na anasimamia kauli yake kama Masheikh wa UAMSHO hawana hatia, waachiwe. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
CCM imesema hawatasita kuwafukuza ndani ya chama hicho watuhumiwa wa kashfa mbalimbali ambazo zimeisababishia nchi hasara. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Serikali imetakiwa kukusanya mapato ili kutatua matatizo ya jamii na ihamasishe jamii kulipa kodi ili kutekeleza Bajeti yake. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Mbowe amesema kauli za kisiasa na kibabe hazifai kutumiwa kumaliza mauaji ya raia wasio na hatia Kibiti, Rufiji na Mkuranga. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Zaidi ya magari 103 yanashikiliwa Njia Panda na Himo, Kilimanjaro yakiwa yamebeba mahindi tayari kusafirishwa nchini Kenya. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
NGOs zimempinga JPM kuhusu watoto wajawazito kutorudi shule wakijifungua zikisema ni kinyume cha sheria na haki za watoto. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) June 30, 2017
Mambo 7 CCM imeyazungumza!!!