Issue ya kushikiliwa mfayabiashara maarufu Yusuf Manji na Jeshi la Polisi DSM ni moja ya story ambayo inaendelea kumake headlines katika mitandao mbalimbali lakini pamoja na hayo nimekukusanyia story kubwa 25 ambazo zimepewa uzito mkubwa.
Hizi ni Tweets 25 za story kubwa asubuhi ya leo July 5, 2017 ambazo zimejadiliwa kwenye Magazeti ya Tanzania.
Wafanyabiashara wa mazao ya chakula wametakiwa kuacha tabia ya kusafirisha chakula nje ya nchi bila kufuata taratibu za Serikali. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Wizara ya Habari imeahidi kutoa ushirikiano wa kitaalamu na kisera kukuza kituo cha utamaduni Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Kambi Rasmi ya Upinzani imesema haipingi jitihada kuokoa rasilimali bali haikubaliani na miswada kuwasilishwa kwa hati ya dharura. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Jeshi la Polisi Simiyu limewataka madereva wa pikipiki na magari kuhakikisha wanakuwa na vyeti vinavyoonesha kusomea udereva. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Serikali imetangaza kutoa ajira mpya 3,000 katika sekta ya Afya zikihusisha wataalamu mbalimbali wakiwemo madaktrari na wauguzi. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
"Lazima mali za watu masikini ziende kuwanufaisha watu, ndio haki yao." – Rais Magufuli. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
M/kiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili Prof. Lipumba amesema Katibu Mkuu Maalim Seif hana mamlaka ya kufungua kesi dhidi ya Rita #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Uchunguzi wa tuhuma za kushambuliwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Juliana Shonza unaendelea huku Wabunge 7 wa CHADEMA wakihusishwa. #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Mfanyabiashara Yusuf Manji na wenzake wawili wamewasilisha maombi Mahakama Kuu wakiiomba iiamuru Polisi iwashtaki au iwaache huru #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee amekamatwa kwa amri ya DC huku viongozi wengine wa chama hicho Tabora wakifungwa mwaka mmoja #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Serikali imeendelea kutafuta njia za kudhibiti rasilimali baada ya sheria kupendekeza mambo 6 kufanya mapinduzi katika madini. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Wajasiriamali wameiomba Serikali kujenga mazingira ya ulipaji kodi na malipo anuai ya vibali vya biashara ili kuondoa urasimu #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Wauza nguo 200 wa jumla na rejareja Mwanza wamemlalamikia Mkurugenzi kwa kupandisha tozo na ushuru bila kuwashirikisha. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini Lema (CHADEMA) kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirishwa hadi Sept. 19. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Acacia imewasilisha Serikalini notisi ya majadiliano kwa niaba ya kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Bulyanhulu. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Mkazi mmoja wa Kimara Temboni amefikishwa mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 16. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Uongozi wa CHADEMA Morogoro umemsimamisha Katibu wake wa Wilaya ya Morogoro Mjini ambaye analalamikiwa kuwatapeli baadhi ya watu. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Rais mstaafu Mzee Mwinyi amesema hana shaka na TZ kufikia uchumi wa viwanda kwa kuwa hali inatia moyo na kuonesha matumaini. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Serikali imesema inatambua changamoto ya upungufu wa masoko ya uhakika kwenye mazao ya chakula kinachozalishwa kwa ziada hapa nchini. #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Wananchi na wageni wameonywa kutojihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwa kuwa hakuna atakayebaki salama dhidi ya mkono wa Dola. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Polisi DSM inamshikilia mfanyabiashara Yusuf Manji kwa tuhuma za kukutwa na nyara za Serikali, mali ya Jeshi la Wananchi. (JWTZ). #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Serikali imeufuta Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), majukumu yake yatahamishiwa kwa Kamishna wa Madini ambayo itaanzishwa. #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
DC Kongwa ameagiza Polisi kuwaweka mahabusu wauguzi wanne wa Hospitali ya Wilaya hiyo wakidaiwa kusababisha kifo cha mtoto mchanga. #MAJIRA
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Shirika la Hali ya Hewa Duniani limeuingiza Mt. Kilimanjaro ktk nchi zenye milima yenye barafu ikiwa ni utaratibu wa Shirika hilo. #MAJIRA.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
Imeelezwa kuwa utoaji wa huduma za afya usiozingatia ubora huathiri kila mtu sio tu wateja na wagonjwa bali hata watoa huduma. #MAJIRA.
— millardayo (@millardayo) July 5, 2017
FULL VIDEO: Prof. Lipumba afunguka, ajibu tuhuma alizotoa Maalim Seif!!!